UMATI umefurika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza utetezi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.
Awali upande wa utetezi uliiambia Mahakama kuwa una mashahidi wanne akiwamo mshitakiwa mmoja wa uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Bosco Kimela.
Liyumba anayekabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya yanayohusu ujenzi wa majengo pacha ya BoT, anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jopo la mawakili linalomtetea Liyumba limewasilisha orodha ya vigogo watakaomtetea iliyosainiwa na wakili Majura Magafu. Miongoni mwa watakaotoa utetezi ni Liyumba mwenyewe.
Wengine ni Mkaguzi wa Hesabu wa BoT, Rashid Mwanga; aliyekuwa Katibu wa Bdi ya Wakurugenzi, Bosco Kimela na Elias Isangya aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha katika benki hiyo.
Liyumba anakabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya madaraka. Utetezi wake utafanyika mbele ya jopo la mahakimu Lameck Mlacha, Benedict Mwingira na Edson Mkasimongwa.
Mahakama ilimuona Liyumba ana kesi ya kujibu juu ya mashitaka yanayomkabili ya kuisababishia hasara Setikali ya sh. bilioni 221/.
Hasara hiyo ilitokana na ujenzi wa majengo pacha yaliyojengwa BoT. Hadi tunakwenda mitamboni kesi hiyo ilikuwa bado haijaanza kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment