header

nmb

nmb

Thursday, April 22, 2010

PINDA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA UCHAGUZI MKUU UJAO!!

MZEE PINDA ALIPOKUWA AKINCHINI KAGUA GWARIDE HUKO MBELE.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema hakutakuwa na mwingiliano wowote katika siku ya Uchaguzi Mkuu kama ambavyo baadhi ya watu amekuwa wakifikiria na kuwataka Watanzania kushiriki.

Akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Manju Msambya, katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, kuwa Serikali haoni kuwapo kwa mwingiliano na shughuli za dini katika siku hiyo.

“Sioni sababu za mwingiliano wa shughuli za dini kwani siku hiyo upo muda wa kutosha ili kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anashiriki kwenye uchaguzi,” amesema Pinda.

Amesema ana imani kuwa siku hiyo shughuli mbalimbali za maendeleo hazitawea kusababisha wananchi kutoshiriki kwenye uchaguzi ili kuwachagua viongozi wanaowapenda na kuwaamini kwa ajili ya kuwatatuliwa kero mbalimbali.

Wakati huo huo, Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Halima Mdee, ameitaka Serikali kutoa tamko kuhusiana na viongozi wake kuchafuliwa kuhusiana na kutumia vyeti vyeti na mwanaharakati Msemakweli.

Hata hivyo Spika wa Bunge Samuel Sitta aliingilia katia na kusema kuwa tayari suala hilo lipoa mahakamani hivy Waziri hatoweza kulijibu.
Mwisho

No comments:

Post a Comment