MWIMBAJI Mary J. Blige amekana taarifa iliyoandikwa na jarida moja nchini Marekani Marie Claire likidai kuwa na ujauzito.
Katika jarida hilo, Blige alisema kuwa alipongezwa na mwandishi wa jarida hilo kwa kuwa tayari kuzaa na mumewe Kendu Isaacs ambapo mtoto wao wa kwanza hakuwa rizki.
"Katika jarida la Marie Claire, ilielezwa kuwa Mary J. Blige anatarajia kupata mtoto na mumewe kipindi hiki cha majira ya joto," liliandika jarida hilo.
Mwanadada huyo amekuwa katika mizunguko yake kikazi kutokana na kupata mialiko mingi na kwamba anaendelea vizuri kwa sasa huku akisisitiza kuwa hana ujauzito.
Rihanna azidi kutesa namba 1
KWA wiki tano sasa mwanadada Rihanna anashikilia nafasi ya kwanza kutokana na kibao chake cha "Rude Boy" katika chati za Billboard 100.
"Rude Boy" ni miongoni mwa nyimbo zinazotengeneza albamu ya "Rated R" ambayo aliitoa mwishoni mwa mwaka uliopita nchini Marekani.
Rihanna mwishoni mwa wiki aliungana na wanamuziki mbalimbali akiwemo Mary J. Blige, Jill Scott na Erykah katika maonesho yao mbalimbali nchini humo.
Rihanna kwa sasa ni miongoni mwa wasichana walio katika nafasi ya juu katikia mauziki ambapo amekuwa na safari pamoja na mialiko mbalimbali ndani na nje ya Marekani.
Katika siku za hivi karibuni, Rihanna anatarajiwa kutangaza safari ndani ya majira haya ya joto.
Monica ajutia wimbo wake!!
MWIMBAJI wa muziki wa R&B na Pop nchini Marekani Monica, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la "Everytime The Beat Drops".
Imeelezwa kuwa miongoni mwa maneno yaliyomo katika kibao hicho yanaonekana kudharau baadhi ya watu kitu ambacho wapenzi wa muziki hasa Marekani wamelalamikia.
" Kama ningejua, wala nisingethubutu kutoa kibao hicho," alisema Monina wakati akizungumzia mipango yake ya wiki ijayo.
Kibao hicho cha "Everytime The Beat Drops" kilichopo katika albamu aliyoitoa hivi karibuni ijulikanayo kwa jina la "Still Standing".
"Mambo mengine yanayoweza kutokea kwa mtu si lazima yatokee kwangu muimbaji, katika albamu yangu ya hivi karibuni nilitaka kuonesha utofauti na zile za awali" alisema Monica.
No comments:
Post a Comment