header

nmb

nmb

Friday, April 23, 2010

HATIMAYE MKATABA WA MRADI WA UENDELEZAJI WA ENEO LA MAKAZI BORA. MCHIKICHINI ILALA DSM WATIWA SAINI!!


Mchoro wa Majengo yatakayoota kama uyoga Ilala Mchikichini siku chache zijazo kuanzia leo
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ramadhan K. Dau akitia saini sambamba na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika hilo Bw. Abubakari Rajabu (Kushoto). Bw.Dau aliueleza umati uliofurika katika eneo hilo kuwa atahakikisha shirika lake halita kuwa na kikwazo katika kupeleka puta mradi huo

Mstahiki Meya wa Ilala Abuu Juma (kushoto) Akianguka sambamba na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Gabriel K.B. Fuime wakati wa hafla hiyo. Wanaoshudia (kushoto) nyuma ni naibu Meya Jerry Slaa na Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia ujenzi huo Bi. Ritta Kabati.

Bw.Mahamed Hussein ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya SUMMETRICC LINK(SDN)-BHD, naye alianguka wino kama mjenzi Mkuu wa nyuba hizo

Baadhi ya wananchi wakiangalia Ramani hiyo



Mstahiki Meya piya akiduwaa kuona mambo muruuuwaa!!!!
Diwani wa Kata husika Rupilia (katikati) akishushia soda baada ya kuona Mradi umeiva. Kwa sasa amejiweka ktk nafasi nzuri ya kushinda tena nafasi yake

Madiwani na wadau wa mradi
Pia kulikuwa na Burudani ya Ngoma za jadi.
HOTUBA
MRADI WA UENDELEZAJI WA ENEO LA MAKAZI BORA. MCHIKICHINI, ILALA DAR ES SALAAM
WAGENI WAALIKWA
1. Mhe. Meya 2.Waheshimiwa Madiwani
3.Mhe. Mwenyekiti wa CCM Wilaya
4.Mhe. Katibu Mkuu wa CCM Wilaya
5.Mhe. Mwenyekiti wa bodi ya NSSF
6. Mhe. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
7. Wawakilishi wa kampuni ya Symetric Link ya Malaysia
8.Kamanda wa polisi kanda maalumu
9.Kamanda wa polisi Mkoa wa Dar es saalam
10. Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco
11.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba la Taifa
12.Mkurugenzi Mkuu wa Dawasco
13.Mkurugenzi Mkuu wa Dawasa
14. Wageni waalikwa
15. Mabibi na Mabwana

Kwa muda mrefu Manispaa ya Ilala ilitafuta mwekezaji wa kuendeleza eneo la Mchikichini Ilala bila mafanikio, hatimaye Manispaa imefanikiwa kuungana na shirika la nyumba la Taifa la Hifadhi ya Jamii na kampuni ya Symetric Link ya Malaysia katika kufanikisha mradi huu.

Eneo hili lina wakazi wasiopungua 400 ambao wapo katika nyumba zilizo kwenye hali mbaya, wakazi hawa watajengewa maghorofa ndani ya eneo hilo ili kupisha ujenzi wa majengo yatakayouzwa kibiashara.

Mradi huu utahusisha majengo yafuatayo:
a) Maghorofa ya bei nafuu ya flati 400 zenye urefu wa ghorofa 17.

b) Maghorofa ya bei za wastani ya flati 1, 195 zenye urefu wa ghorofa.

c) Maghorofa ya bei za juu yenye flati 604 zenye urefu wa ghorofa 35

d)Majengo matatu ya ofisi yenye urefu wa ghorofa 25

e)Hoteli ya kimataifa zenye urefu wa Ghorofa 50

F)Hoteli ya ngazi ya kati: zenye urefu wa ghorofa 10

g)Sehemu ya kisasa kwa ajili ya maduka yenye ghorofa 3.

h)Ofisi ya Halimashauri ghorofa 40

Hatua za awali
1. Ujenzi wa awamu ya kwanza utahusisha ujenzi wa maghorofa 2 yenye urefu wa ghorofa 17 kila moja ambayo yatakuwa na jumla ya nyumba 480.

Awamu ya kwanza utahusisha ujenzi wa maghorofa ya nyumba za makazi ikiwa ni pamoja na maghorofa ya bei nafuu ili kupisha eneo la mradi.

Nyumba hizi zitatolewa kwa kuuzwa kwa bei nafuu kwa wakazi wa eneo la Mchikichini watapata nyumba na hakuna hata mmoja atakaye kosa.

2. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa majengo ya biashara, maofisi na hoteli. mradi huu utatekelezwa ndani ya muda wa miaka minne hadi mitano.

Nyumba hizi pamoja na majengo ya biashara, ofisi na hoteli zitauzwa kwa umma wa Tanzania.
Mradi utachangia katika kuleta maendeleo kwa wakazi wanaozunguka eneo hilo na kwa Taifa zima. Faida za mradi huu ni pamoja na kutoa makazi bora, ajira kwa vijana na kuchangia katika pato la taifa.

Ningependa kuuhakikishia umma kwamba mradi huu mkubwa wa aina yake utakuwa ni chachu ya maendeleo na vilevile katika kutekeleza adhima kubwa ya Serikali ya makazi bora kwa kila Mtanzania na Halimashauri ya Manispaa ya Ilala na kisha katika nchi nzima.

No comments:

Post a Comment