header

nmb

nmb

Friday, April 23, 2010

BOSS WA WORLD WIDE MORVERS AFIA HOTELINI

MSHAURI wa kampuni ya World Wide Movers Kandasamy Govindha Rajan (57), mwenye asili ya Kiasia amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ya Ekono iliyopo mtaa wa Libya Kariakoo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu maiti hiyo iligundulika jana saa moja jioni katika chumba namba 304 baada ya wahudumu wa hoteli hiyo kutomuona mgeni huyo tangu kulipokucha.

Ilidaiwa kuwa, baada ya kusubiri kwa muda merfu bila kutokea waliamua kuvunja mlango na kubaini mgeni huyo akiwa amekufa huku maiti yake ikiwa imelala kitandani.
Pia mezani kwake kulikutwa dawa za aina mbalimbali alizokuwa akizitumia ambapo inadaiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao bado haujafahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa, jeshi lake linaendelea na upelelezi.

Akizungumza kwa njia ya simu jana asubuhi alisema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo alikuwa akisumbuliwa na malaria ambapo alifika hotelini hapo Aprili 20, mwaka huu na alikuwa akilalamika kuumwa.

Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Muhimbili na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment