header

nmb

nmb

Friday, April 23, 2010

MWANAFUNZI KIZIMBANI KWA KUFANYA FUJO OFISI ZA ITV!!!

MWANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kisarawe Asha Juma (17), mkazi wa Mbagala amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashitaka ya kumfanya fujo katika kituo cha televisheni cha ITV.

Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa, kituo cha ITV kilimuahidi kumpatia fedha taslimu Sh. 800,000 kwa ajili ya ada ya shule lakini wao walimpatia Sh. 600,000 tu tofauti na ahadi yao waliyoitamka hapo mwanzo.

Kesi hiyo ilikuwa mbele ya Hakimu Anna Mshigwa na kusomwa na Karani Emakulatha Philipo kuwa, Aprili 16, mwaka huu, mshitakiwa alifanya fujo katika kituo hicho.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 29, mwaka huu.
Pia, Juma Ally (25) na Fatma Kassimu (28), wakazi wa Mwananyamala wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashitaka ya kukamatwa na kete tano za bangi.

Mbele ya Hakimu Mary Matoi imedaiwa na Karani Fatma Khatibu kuwa, Aprili 18, mwaka huu, washitakiwa walikamatwa na askari wakiwa na kete 5 za bangi walipokuwa doria maeneo hayo.

Washitakiwa wamekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 29, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment