JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mzazi Kimoma Martin (37), kwa tuhuma za kumuingilia kimwili mtoto wake wa kike wa kumzaa wa miaka 12.
Akisimulia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Masimbe amesema kuwa, mzazi huyo alishikiliwa na polisi baada ya mtoto wake kufichua siri kwa mama yake wa kambo kuwa, mbona baba yake huyo humuingilia kimwili.
Amesema kuwa, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Kijichi alikuwa akiishi na baba yake huyo baada ya mama yake kufariki mwaka 2008.
Ameongeza kuwa baada ya mzazi huyo kufariki baba huyo alianza kufanya mapenzi na mtoto huyo ambaye kwa maelezo yake aliona kuwa ni jambo la kawaida hakujua kama lina madhara.
Kamanda amesema kuwa, baada ya walimu kuanza kutoa semina juu ya mambo ya UKIMWI na ngono zembe kuwa hazifai kwa wanafunzi ndipo mtoto huyo aliposhtuka na kuanza kueleza kuwa mbona yeye baba yake huwa anamuingilia kimwili.
Kutokana na hali hiyo mtoto huyo alikwenda moja kwa moja kumueleza mama yake wa kambo ambaye aliamua kutoa taarifa polisi na ndipo baba huyo aliponaswa.
Mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na Polisi na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Katika tukio lingine, mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu Berita Frank amekufa baada ya kugongwa na gari katika ajali iliyotokea Keko Mwanga.
Kamanda Masimbe amesema kuwa, ajali hiyo imetokea jana saa 8 mchana, Keko Mwanga.
Amesema kuwa, ajali hiyo ilisababishwa na gari T
271 AJE aina ya Toyota Carina iliyokuwa ikiendeshwa na Alfan Ngarambe ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Temeke.
No comments:
Post a Comment