FAMILIA ya Lucas Lutara wakazi Polisi Ufundi imeshikwa na butwaa baada ya mtoto Laitnes Lucas (20), kuchukuliwa na mtu asiyefahamika wakati akicheza nje ya nyumba na watoto wenzake.
Akizungumza na gazeti hili baba wa mtoto huyo Lucas Lutara amedai kuwa kutekwa kwa mtoto wake anahisi kuwa kumetokana na kuripishana kisasi ili kumkomoa.
Amesema kuwa akiwa nyumbani kwake jana huku mtoto wake akicheza nje alisikia mtoto wake wa kike akimweleza kuwa, mdogo wao haonekani.
Amedai kuwa baada ya kwenda kumuangalia kwa majirani walibaini kupotea kwa mtoto huyo na ndipo jirani wao alipowaeleza kuwa amemuona mtoto huyo akiwa amebebwa na kijana mmoja akienda maeneo ya Keko Juu.
Ameongeza kuwa kijana huyo inadaiwa kuwa alikuwa amevaa tisheti mbili ambapo majirani waliamua kuanza kumfutilia lakini jitihada zimekwama hadi leo.
Taarifa za kutekwa kwa mtoto huyo zimetolewa katika kituo cha Polisi Kilwa Road na kupewa namba KRL/RB/1700/2010.
Baba huyo amesema kuwa, hata hivyo anamuhisi kijana mmoja ambaye alikuwa ni mume wa msichana wao wa kazi ambaye waliachana baada ya ugomvi kukithiri kati yao.
Amedain kuwa, baada ya kijana huyo kubaini msichana huyo anaishi katika nyumba yao ndipo alipoanza kufika mara kwa mara na kumshambulia.
" Kitendo kile mimi kilinikera kwani ilinibidi nimkamate kijana yule ili kukomesha tabia za kumfuata msichana wangu wa kazi kwani alikuwa akimtesa kwa kumpiga jambo ambalo naona lilimkera kijana huyo na ndiyo maana nahisi ameamua kunifanyia unyama huu kwa lengo la kunikomoa,"amesema Lucas.
No comments:
Post a Comment