header

nmb

nmb

Friday, April 9, 2010

SASA LIYUMBA ATAJIBU STAKA 1 BADALA YA 2. JOPO LA MAHAKIM WASEMA KOSA LA HASARA HALINA USHAHIDI WA KUTOSHA



NDUGU na jamaa leo asubuhi walifurika katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa mahakama kama itamwachia huru ama la aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.

Mshtakiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo na basi la Magereza lenye namba usajili STK 4373.

Mbalia na wana ndugu hao kufurika mahakamani hapo pia idadi ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia walionenaka kuwa wengi kwa ajili ya kujua hatma hiyo.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia Serikali hasara ya sh bilioni 221.

Kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu ama la baada ya mahakama kumaliza kusikiliza utetezi wa upande wa mashtaka uliotolewa mahakamani hapo.

Upande wa mashtaka ulitoa sababu za msingi kuwa umeona mshtakiwa ana kesi ya kujibu kutokana na mashahidi waliofika mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa.

Awali upande wa utetezi uliiomba mahakama imwachie huru mshtakiwa kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Kutokana na kuwepo kwa malumbano hayo jopo la mahakimu, Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa, ulikubaliana na maombi ya pande zote na kutakiwa kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya maandishi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu ama la.

Katika kesi hiyo Liyumba anatetewa na mawakili Majura Magafu, Hudson Ndusyepo.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya mwaka 2001 na 2006 akiwa ameajiriwa BoT, alitumia vibaya ofisi yake kwa kuchukua uamuzi katika ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.

Katika kosa la pili, mshitakiwa huyo alidaiwa kuwa kati ya kipindi hicho alitumia vibaya ofisi yake kwa kuidhinisha malipo ya majengo pacha ya BoT bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi hivyo kusababisha hasara kwa Serikali ya sh. bilioni 221.1.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni bado kesi hiyo ilikuwa haijaanza kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment