header

nmb

nmb

Thursday, April 29, 2010

SERIKALI YAWAKOROMEA WAHADHIRI WALIOJIINGIZA KATIKA MGOMO USIO WAHUSU!!


SERIKALI imesema imesikitishwa na hatua ya baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini kutangaza mgomo kwa kuwa ni batili na kwamba wanaodai ni si wote bali ni 62 tu.


Pia Serikali imeahidi kutekeleza matakwa ya wahadhiri hao na kuahidi kulishughulia kwa kuwahamisha kutoka mfuko wa zamani wa Senior Staff Superannuation Scheme (SSSS), kwenda Mfuko Pensheni wa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma (PPF).


Akizungumza jana usiku Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi, amesema Serikali imeazimia kuwahamisha wahadhiri hao na kuwataka kusitisha mgomo wao haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment