header

nmb

nmb

Thursday, April 29, 2010

MAJONZI KIJIJI KIZIMA NI BAADA YA MAMA KUWACHANJA WATOTO WAKE 4 KWA SHOKA NA KUWATOA ROHO!!


VILIO na simanzi vimetawala kijiji cha Rau Moshi baada ya mwanamke mmoja anayedhaniwa kuwa na ugonjwa wa akili kuwacharanga kwa shoka watoto wake wanne.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu hadi leo asubuhi miili ya watoto watatu ilikuwa katika Hospitali ya KCMC huku mtoto mmoja akiwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, mauaji hayo yametokea wakati baba wa watoto hao akiwa kazini.
Imedaiwa kuwa mara baada ya mama huyo kuanza kuwacharanga kwa shoka, watoto wake walijitahidi kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini hata hivyo ilishindikana.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, amesema leo asubuhi kuwa tukio hilo lilitokea jana jioni.
Amesema miili ya watoto hao ilikutwa na baba yao Thadei saa 12 leo asubuhi ndani ya nyumba eneo la Kariwa chini Kata ya Longuo. Thadei anafanya kazi ya ulinzi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Alimtaja mama wa watoto hao kuwa ni Benedicta Thadei (44) na kwamba aliwakatakata kwa shoka watoto hao usiku wa manane wakati baba wa watoto hao akiwa akiwa kazini. Amesema watoto waliouawa ni Noela Thadei (5), Anthony Thadei (2) na Rose Thadei (12), ambaye ni mlemavu wa akili na viungo ambaye alikuwa akilelewa katika kituo cha kulelea walemavu kilichopo karibu na Rau Msikitini. Aidha alisema hali ya mtoto Paskal Thadei (9), anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Moshi, amejeruhiwa kwa kukatwa na shoka kichwani na amelazwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu. “Marehemu wote hawa wameuawa kwa kukatwakatwa na shoka na mama yao huyo na wote kufariki papo hapo ... mume wa mama huyo aliikuta miili ya watoto wao asubuhi, damu ikiwa imetapakaa nyumba nzima,” amesema Kamanda Ng'hoboko.
Kamanda amesema miili ya watoto hao imehifadhiwa Hospitali ya KCMC na kuwa uchunguzi zaidi unendelea ili kujua chanzo halisi cha tukio hilo na kwamba hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa mama huyo amehusika katika mauaji hayo. Hata hivyo, amesema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na kwamba upelelezi wa awali unaonesha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na historia ya kuugua akili na alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

habarihii pia inapatikana kwenye Gazeti la Dar Leo la leo

No comments:

Post a Comment