header

nmb

nmb

Thursday, April 29, 2010

BIASHARA YA MAUWA YADODA ARUSHA, WAUZAJI WALIA NJAAA!!

D,MATAKA
NDEGE YETU

SEKTA ya utalii na biashara ya maua mkoani Arusha, imeathirika sana baada ya mashirika makubwa ya ndege barani Ulaya, kusitisha safari zao katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.
Kusitishwa kwa safari hizo, kumetokana na mawingu mazito ya mlipuko wa volcano nchini Iceland, ambayo yalifunika nchi za bara la Ulaya kuanzia Magharibi hadi Mashariki.
Idadi ya watalii kutoka Ulaya wanaotembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini nao wamepungua. Hali hiyo imesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utalii.
Akizungumzia athari hizo hivi karibuni, wakala wa utalii mkoani humo Bw. Samwel Lugemalila, alisema milipuko ya volcano imeharibu malengo ya wadau mbalimbali wa sekta hiyo hasa katika kipindi hiki cha msimu wa watalii.
Ofisa kutoka Bodi ya Utalii nchini, (TTB), ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu sio msemaji wa bodi, alisema tatizo hilo limeathiri sekta ya utalii kwa asilimia 30.
“Asilimia zaidi ya 98 ya watalii wanaokuja nchini, wanatoka barani Ulaya wakitumia usafiri wa anga, hivyo kusitishwa kwa safari za mashirika makubwa ya ndege, kumeziathiri sekta mbalimbali,” alisema Ofisa huyo.
Uchunguzi uliofanywa mkoani hapa, umebaini kuwa tani 750 za shehena ya maua na mbogamboga, zimeharibika baada ya kushindwa kusafirishwa katika nchi mbalimbali za Ulaya.
Mfanyabiashara wa sekta hiyo Bw. Paul John, alisema shehana kubwa ilikwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya muda mfupi baada ya safari za ndege kusitishwa.
Mashirika hayo ya ndege, yameanza safari zake baada ya tatizo hilo kwisha. Nchi mbalimbali barani Afrika zimelalamikia hasara kubwa waliyoipata hasa katika sekta ya utalii tangu kusitishwa kwa safari hizo.

No comments:

Post a Comment