header

nmb

nmb

Thursday, April 29, 2010

ROHO MBAYA DHIDI YA ZELUZELU INAENDELEA, KWANINI WANANCHI HAWATAKI KUELIMIKA!!

HAWA NI SEHEMU YA VIONGOZI WANAOPINGA MAUAJI NA UBABE KWA ALBINO NCHINI.

Kahama
Albino msichana Kabula Nkarango(13) wa kijiji cha Luhaga kata ya Igwamanoni Kahama amekwatwa mkono juzi saa tano usiku akiwa amelala na mama yake.


Bw. Emmanueli Nkarago alisema mtoto huyo alikatwa akiwa amelala ndani ya nyumba na mama yake Bi. Limi Mwambilija ambapo watu hao waliokuwa zaidi ya wanne walikuwa na bunduki ambayo hawakuweza kuitambua na kuingia ndani kwa kuvunja mlango.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bi. Bahati Matala alisema watu hao walipoingia yalidai pesa kwanza, akielezea kaka yake na Albino, Bw. Emmanueli Nkarango alisema baada ya kumkata waliuliza mama yake kama ana mafuta ya taa alijibu hana ndipo yalipokwenda kwenye kibanda cha duka la kaka yake na kukivunja na kuchukua mafuta .


Bi. Matala alisema baada ya kuchukua mafuta walimlazimis mama yake kumpaka sehemu waliyoikata ili kuzuia damu kutoka ili asife huku watu hao wakimsaidia kumfunga majeraha walipomaliza na kuchukua mkono.


Alisema kuwa walimwambia huyo mama asiwalaumu kwa kuwa wanatekeleza ya mtu aliyewatuma pia usiku huo walikwenda kuvamia kwa watu wengine wawili wenye maduka kijijini hapo kuvunja na kupora na kuwajeruhi vibaya.


Kamanda wa Polisi Mkoani hapo Bw. Daudi Sias alisema kuwa albino huyo amekatwa mkono wa kulia na jeshi la polisi linaendelea na msako kuwatafuta watu hao na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kahama, Dkt. Leornad Subi alisema albino huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama huku akiwa ameongezewa damu chupa mbili.

No comments:

Post a Comment