header

nmb

nmb

Friday, April 30, 2010

MWEMA UPO POLISI ATUHUMIWA KUBAKA MWANAWE WA KUMZAA!!!Zaidi pata Dar leo ya leo.

IGP MWEMA.

WAKAZI wa Ireje mkoani Mbeya juzi walishikwa na butwaa baada ya kusikia mayowe kutoka kwa jirani yao aliyekuwa akiomba msaada baada ya kumfuma mumewe akimuingilia kimwili mtoto wa kumzaa mwenyewe wa kike wa miaka tisa.
Kutokana na mayowe hayo umati ulijitokeza kutoa msaada ambapo wananchi wenye hasira kali walimvamia hali iliyosababisha baadhi ya watu kupiga simu polisi ili kuokoa jahazi.
Muda mchache baadaye polisi walitinga eneo la tukio na kumuokoa mwenzao ambaye amefahamika kwa jina la Koplo Robert.
Baadhi ya wananchi waliongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamedai kuwa, huenda askari huyo alikuwa akimuingilia mwanaye kimwili kutokana na imani za kishirikina.
Imedaiwa kuwa, baadhi ya majirani waligundua mchezo huo mchafu uliokuwa ukifanywa na askari huyo tangu zamani baada ya kumsikia mtoto huyo akilalamikia maumivu mara kwa mara hali iliyowatia hofu majirani hao.
Imedaiwa kuwa, baba huyo alikuwa akimfunga mdomo mtoto huyo pindi anapotaka kumuingilia kimwili ili asipige kelele.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi amethibitisha kushikiliwa kwa askari huyo.
Hata hivyo Kamanda Nyombi amesema kuwa, wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa madai ya kumfanyia shambulio la aibu binti yake huyo wa kumzaa.
"Inadaiwa kuwa askari huyu alikuwa akimuingiza vidole sehemu za siri binti yake hivyo tunafanya uchunguzi wa kina na baada ya kukamilisha upelelezi hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,"amesema Kamanda Nyombi.

No comments:

Post a Comment