header

nmb

nmb

Wednesday, April 28, 2010

KANISA LA KAKOBE LATEMA CHECHE MBEYA KWA VIBAKA NA WACHAFUA AMANI NCHINI!!

ASKOFU WA KANDA YA MBEYA
Na Thompson Mpanji,Mbeya

KANISA la Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F) limelaani vikali mauaji ya watoto wadogo yanayohusishwa na imani za kishirikina yaliyotokea hivi karibuni katika Wilaya ya Rungwe,Mbarali na jijini Mbeya pamoja na kusitisha maovu hayo sanjari na ajali zilizokuwa zikitokea mara kwa mara na kugharimu maisha ya watu.

Maombi ya kumuomba Mungu asitishe vitendo viovu vinavyohusishwa na imani za kishirikina,ajali za barabarani,uhalifu wa aina mbalimbali yalifanyika na kuchukuwa muda wa masaa sita kuanzia saa 3 hadi saa 8 mchana katika kanisa hilo lililopo maeneo ya Block T,jijini Mbeya.

Askofu wa kanisa la F.G.B.F Jimbo la Mbeya,Mch.Kingstone Mwaijande ambaye aliongoza ibada hiyo ameyalaani kwa nguvu zote mauaji ya ajabu yanayoendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya na kwamba kupitia ibada hiyo wamemuomba mwenyezi mungu kusitisha ili yasiendelee kutokea tena.

“Kama mtumishi wa mungu nasimamisha mauaji ya watoto kuanzia leo hamtasikia tena na washirikina na wachawi atakayethubutu kufanya mauaji atakufa na kama kuna mtu anabisha na kupinga ajaribu aone…nataka kusikia Mbeya mjini ipo salama,Mbarali,Rungwe,Kyela,Mbozi,Chunya na Ileje alikadhalika,”alisema.

Alisema kama zama za mababu,Simon Mchawi na Elima walishindwa kwa Paulo na Philipo kutokana na nguvu za mwenyezi mungu basi hata yeye (Askofu) kama mtumishi wa bwana ameyasimamisha mauaji hayo na kuwaomba waumini wake waendelee kuomba mungu ili aweze kuyaepusha maovu hayo.

“Shetani hawezi kunifanya kitu nina Yesu aliye hai,ninyi leo ni mashahidi imefika wakati kanisa la mungu liinuliwe,kanisa wajibu wake kuomba ili yasitimie maovu na wenye watoto wasisononeke,waliotenda washushiwe gharika,”alisema.

Aidha alisema endapo mchakato wa uchaguzi mkuu ndiyo unaleta mauaji basi upite salama na roho za ushirikina,ajali za magari zinazogharimu maelfu ya watanzania zikome pamoja na ujambazi,wizi na upigaji nondo.

Hata hivyo Askofu huyo ameiomba serikali kuwashirikisha viongozi wa dini katika masuala kama hayo na kwamba yeye yupo tayari kushirikiana nao endapo watahitaji msaada wake katika kuhakikisha Mbeya inabaki

No comments:

Post a Comment