header

nmb

nmb

Wednesday, April 28, 2010

BABA SITTA UMEIONA HII... MAYAI YALITOKA WAPI BUNGENI??


Wasaidizi wa Spika wa bunge la Ukraine wakimfunika kwa mwamvuli spika huyo,Bw. Lytvyn asipigwe kwa mayai baada ya kuibuka ghasia ndani ya ukumbi wa bunge hilo jana.

Ghasia zaibuka Bunge la Ukraine
* GHASIA zimeibuka ndani ya Bunge la Ukraine baada ya bunge hilo kupitisha hatua ya Urusi kuendelea na shughuli zake katika kituo cha jeshi la wanamaji cha jeshi la nchi hiyo kilichopo katika bahari nyeusi.

Ghasia hizo ziliibuka jana wakati wa majadiliano kuhusu hatua hiyo hali ambayo iliwafanya Wabunge kupigana, huku Spika akilazimika kujificha chini ya mwamvuli baada ya wabunge kuanza kumpiga kwa mayai.
Hali hiyo ililazimisha pia kutumika mabomu ya kutoa machozi nje ya jengo la bunge hilo.
Wakati ghasia zikiendelea ndani ya Bunge,nje ya jengo hilo Polisi walipambana na maelfu ya waandamanaji huku baadhi yao wakiunga mkono hatua hiyo ama kupinga makubaliano ya wiki iliyopita kati ya marais wa Ukraine na Urusi ya kuongoza muda zaidi katika Urusi kukimiliki kituo hicho cha kijeshi cha Crimea.
Makubaliano hayo ambayo yanaonekana kukuza uhusiano baina ya Urus na Ukraine ni kutokana na kuchaguliwa rais wa Ukraine ambaye anamuunga mkono Rais wa Urusi,Bw. Viktor Yanukovych mwezi Februari mwaka huu lakini unapingwa na wapinzaninchini Ukraine ambao wanapinga siasa za Magharibi.
Habari kutoka nchini humo zilieleza kuwa mapigano yalianza wakati wabunge wakijadiliana kuhusu makubaliano ambayo yalifikiwa kati ya Bw. Yanukovych na Rais wa Urusi,Bw. Medvedev .
Katika ghasia hizo wabunge wa upinzani walimrushia mayai Spika wa Bunge Bw. Volodymyr Lytvyn hivyo kumlazimu kujificha chini ya mwanvuli.
Mbali na Spika pia naibu wake alionekana akipiga ngumi juu ya meza huku akijifunika uso naleso ili kujizuia moshi.
Hata hivyo pamoja na ghasia hizo majadiliano yaliendelea na mkataba huo ukaungwa mkono na wabunge 236 kati ya 450 waliokuwa ndani ya bunge hilo.(BBC)

No comments:

Post a Comment