header

nmb

nmb

Friday, February 12, 2010

Yasemavyo Magazeti ya hapa nchini leo

Muswada gharama za uchaguzi wapita kwa mbinde
MWANANCHI :
Muswada wa sheria za gharama za uchaguzi jana ulipita kwa mbinde huku ukiibua malumbano makubwa baina ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Fredericki Werema na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge pamoja na wabunge wengine kuhusu vipengele mbalimbali vya muswada huo.

Mwanasheria Mkuu wa serikali alipingana wazi wazi na Chenge aliyekuwa mwanasheria mkuu wa zamani hali iliyomlazimu naibu spika kuingilia kati mara kwa mara.

Hakuna mgombea binafsi - Serikali
JAMBO LEO :
Serikali imesema hakutakuwa na mgombea binafsi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Msimamo huo ulitolewa jana na Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo mjini Dodoma ndani ya Bunge wakati akisoma muswada wa sheria ya uchaguzi.

Mafisadi wa elimu 'waitwa ' TCU
MAJIRA
:
Mawaziri wanaodaiwa kughushi vyeti vya taaluma (mafisadi wa elimu) na wengine wanaotiliwa shaka wamepewa nafasi ya kuwasilisha vyeti vyao kwenye Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili kuthibitishwa na kuondoa utata katika jamii juu ya uhalali wa shahada zao, hasa walizozipata nje ya nchi.

Tamko hilo la TCU linakuna siku moja baada ya Spika kumtakasa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Davidi Mathayo kuwa elimu yake haina utata, hivyo watu waache kumzongazonga, lakini hakugusia vigogo wengine wanaodaiwa kuwa na ama vyeti feki au kusoma kwenye vyuo visivyotambulika.

Mdogo wa Lowassa mbaroni
TANZANIA DAIMA :
Mdogo wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Joseph Ngoyai Lowassa na wenzake watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za rushwa.
Joseph na wenzake ambao wote ni askari polisi wa kituo cha polisi Mto wa Mbu wilayani Monduli, wanatuhumiwa kuruhusu shehena ya miti aina ya misandare iliyokamatwa na askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).






No comments:

Post a Comment