Nahodha wa timu ya Chelsea, John Terry jana usiku alitua Dubai akiwa katika harakati za kujaribu kupata sualuhu na mkewe ambaye aliondoa Uingereza wiki mbili zilizopita baada ya kuibuka kwa skendo yake ya kutembe nje ya ndoa.
Terry aliyeonekana kuwa na mawazo mwenye umri wa miaka 29, alipokuwa uwanja wa ndege alionekana 'akipombeka' kwa kunywa pombe kali alikwenda uwnajani hapo kwa gari lake la kifahari aina ya BMW.
Baada ya kuwasili katika eneo la ufukweni ambako mkewe amepanga akwia na watoto wao pacha wennye umri wa miaka mitatu aliweza kutoa tabasamu kidogo .
Terry, alivuliwa beji ya unahodha wa timu ya Taifa ya soka ya England kufuatia skendo hiyo ya kufanya mapenzi na mke wa zamani mchezaji mwenzie wa England, hakupata mapokezi ya shangwe alipowasili Dubai.
Toni mwenye umri wa miaka 28, hakuwepo uwanja wa ndege kumpokea au katika eneo la mbele ya hoteli ya Le Royal Meridien .
Terry akiwa na mawazo ataungana na watoto wake pacha Georgie John na Summer Rose ambao Jumatano wiki hii wanaelezewa kuwa aliangua lilio kutokana na kummisi baba yao.
Kutokana na kulia kwa watoto hao mama yao alifanya jitihada za kufunga milango ili kelele zao zisisikike.
Terry hajakuwa na familia yake tangu kujulikana kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na Vanessa Perroncel, ambaye ni mke wa zamani wa rafiki yake na mchezaji mwezie katika timu ya England, Wayne Bridge.
Leo Toni na Terry wataanza jitihada za kuweka sawa mambo yao kwa ajili ya maisha mazuri ya baadaye pia wanatarajiwa kuwa na kikao cha kifamilia pamoja na wazazi wao.
Kama Terry atafanikiwa kumshawishi anaweza kurejea na mkewe Uingereza na kuwa na kipindi kizuri katika siku ya wapendanao kwa kuwa nao pamoja.
No comments:
Post a Comment