header

nmb

nmb

Monday, February 8, 2010

Pilato wa Ole Sendeka kumtishia mtu pastola ahamishwa..!

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha Bw. James Karahemaya ambaye alikuwa anasikiliza kesi ya inayomkabili Mbunge wa Simanjiro Bw. Cristopher Ole Sendeka amehamishwa kikazi.



Bw Sendeka anatuhumiwa kumpiga na kisha kumtishia bastola Mwenyekiti wa vijana wa CCM Mkoa wa Arusha Bw. James Millia Januari 20 mwaka jana katika Chuo cha Ualimu Monduli.


Kuhamishwa kwa hakimu huyo ambaye amehamishiwa katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma kumezua gumzo katika Mji wa Arusha kutokana kusubuliwa kwa uamuzi kesi hiyo ulikuwa utolewe machi 5.



Akizungumza na waandishi Msajili wa Mahakama Mkoa wa Arusha Bw. George Herbert alisema uhamisho huo wa Bw. Karahemaya ni kawaida.



‘Huu ni uhamisho wa kawaida tena amepandishwa cheo ambapo anaenda kuwa Hakimu Mfawidhi Mpwapwa kuhusu suala la kesi ya Sendeka itaendelea kusikilizwa mahakimu wapo wengi siyo yeye tu’ alisema Bw. Herbert.



Alisema kuwa uhamisho wa Bw. Karahemaya ni utaratibu wa kawaida wa mahakama na kesi alizokuwa akisikiliza kama kawaida na hakimu atatakepangiwa kusikiliza kesi hiyo na kuzitolea hukumu.

No comments:

Post a Comment