header

nmb

nmb

Thursday, February 11, 2010

Asante sana ziende kwa Benki ya CRDB kwa kuwa pamoja ktk Blog hii.

CRDB kuuza hisa zilizosajiriwa DSE
KAMPUNI ya Somolon Stockbrokers LTD imeteua benki ya
CRDB kuwa wakala wa biashara ya hisa zilizoorodheshwa
katika soko la Hisa la Dar es Salam (DSE).

Hatua hiyo ilitangazwa Dar es Salam jana na Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei, alipozungumza na
waandishi wa habari kuhusu matokeo ya kibiashara katika
kipindi cha mwaka jana.

Alisema kwa makubaliano hayo kuanzia sasa matawi ya
benki hiyo yatatumika kama vituo vya ununuzi na uuzaji
wa hisa zilizoorozeshwa katika soko la hisa.

Alibainisha kuwa tayari benki hiyo ina wataalam wa
kufanyakazi hiyo katika matawi yake yote nchini. Alitaja
faida za kununua hisa kupitia tawi la benki kuwa ni
pamoja na gharama kuwa za nafuu, mtu anaweza kununua na
kuuuza hisa kupitia tawi la karibu na kupata taarifa za
mauzo, bei na mtu anaweza kuuza hisa zake.

Akizungumzia huduma nyingine mpya ambazo zitakuwa
zikitolewa na benki hiyo, Dkt. Kimei alisema kuanzia
wiki ijayo watu wanaotumia Mastercard wanaweza
kuzitumia kutolea fedha kwenye mashine za ATM za benki
hiyo.

Alifafanua kuwa tayari benki hiyo imepata leseni ya kuwa
wasimamizi wa Mastercard kama ilivyo kwa Tembo
cardvisa.

Alisema baada ya miezi miwili ijayo benki hiyo itakuwa
imeanza kutoa mastercard.
Wakati huo huo matawi mawili
ya benki ya CRDB yaliyopo jijini Dar es Salaam yataanza
kutoa huduma za kibenki kila siku zikiwemo siku za
sikukuu.

Alitaja matawi hayo kuwa ni Vijana, Kariakoo na hivyo
kuungana na lile la Mlimani City katika kutoa huduma za
aina hiyo. Katika hatua nyingine benki hiyo imepata tuzo
inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kutokana na kuchangia mapato makubwa ya kodi.
Mkurugenzi Mtendaji Dr Chalres Kimei (kulia) akizungumza na wanau pamoja na wana habari waliohudhuria mkutano wake katika .Kushoto ni Ofisa wa Benki hiyo


Bi. Tully Esther Mwambapa awaeleza wanahabari kuwa muda wa Maswali umewasia.

Mwana habari kutoka Gazeti la Mwananchi akiomba ufafanuzi wa jambo


No comments:

Post a Comment