header

nmb

nmb

Monday, August 16, 2010

tume ya taifa ya sayansi na teknolojia yatoa tuzo!!

Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010. (Picha na Aron Msigwa wa Meelezo)
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Godfrey Kimarya mgunduzi wa tanuru la mkaa lenye uwezo wa kutoa mkaa mwingi na wenye ubora kwa gharama nafuu leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment