Mkurugenzi wa Tume ya Uchagunzi ya Taifa (NEC) Rajab Kiravu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo kuhusu maadalizi ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini. Amesema kwa sasa Daftari la wapiga kura lina wapiga kura 19,670,631 na kati ya hao wanaume ni 9,834,322 na wanawake ni 9,852,286 amesema kupungua kwa idadi ya wapiga kura kutoka idadi ya awali ya wapiga kura 21,210,187 inatokana na kuondoa wapiga kura waliofariki ambao idadi yao imefikia 243,631 Amesema uteuzi wa wagombea utafanyika agosti 19 mwaka huu na zoezi linaloendelea hivi sasa ambapo wabunge na madiwani wanachukua fomu hizo kwa wakurugezi wa Halmashauri za Wilaya na wagombea Urais wanachukua fomu hizo katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Amesema Kampeni zitaanza rasmi Agosti 20 mwaka huu na mikutano yote inayofanyika hivi sasa haihusiani na tume ya uchaguzi, ambapo pia tume ya uchaguzi itaanza kutoa elimu ya mpiga kura hivi karibuni ambapo tayari imeshachapisha mabango mbalimbali yanayoelezea umuhimu wa kupiga kura. Kuhusu vifaa vya kupigia kura umefuata utaratibu wa sheria ya ununuzi ya serikali na kwa kufuata kanuni zote za kutangaza zabuni za ununuzi ikiwa na baadhi ya vifaa tayari vimeshawasili nchini. Kamati za Tume zitaanzishwa ambazo zitaishauri tume kwa ajili ya changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa zoezi zima la kupiga kura na kununuam vifaa vya Teknohama (IT) kwa ajili ya kuendesha zoezi kwa ufanisi zaidi lakini pia tume itatoa mafunzo mablimbali kwa wasimamizi wote pamoja na maafisa mbalimbali wa tume ya uchaguzi watakaohusika na zoezi zima la uchaguzi.
No comments:
Post a Comment