header
nmb
Wednesday, August 18, 2010
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI!!
Asalaam Aleikhum Wadau, Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya la www.michuzipost.com ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa. Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia kuboresha libeneke hili. Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu kwa muda wote huu. Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la www.michuzi-matukio.blogspot.com . Hivyo wadau Globu ya Jamii itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa mapana na undani zaidi. Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii inavyojionesha http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments . Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea kama kawa. Libeneke hili jipya la www.michuzi.post.com limewezekana kwa ushauri na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw. Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke hili. Muhidin Issa Michuzi Mkurugenzi Michuzi Post Ltd.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment