Na Mwandishi Wetu
MWANDISHI wa habari mwandamizi anayeishi Washington DC, Marekani, Mobhare Matinyi, amempongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA). Akizungumza na Jambo Leo kwa njia ya simu jana kutoka Marekani, Matinyi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa TASWA, alisema anawapongeza wanachama wote wa chama hicho kwa kufanya uchaguzi huo. "Naomba uafikishie salamu za pongezi Pinto na viongozi wote waliochaguliwa kuiongoza TASWA, waandae mikakati endelevu ya kukitoa chama hapo kilipo ili kipige hatua zaidi," alisema Matinyi ambaye pia ni mshauri anayefanya kazi zake Marekani. Pinto ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo, aliibuka mshindi juzi kwa kupata kura 60 kati ya 79 zilizopigwa, akiwabwaga Mhariri wa gazeti la Spoti Starehe, Masoud Sanani aliyepata kura 11 na Mpoki Bukuku wa gazeti la Mwananchi aliyepata kura nane. Pinto amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Boniface Wambura ambaye ni Mhariri Mkuu wa Jambo Leo. Mhariri wa Michezo wa gazeti la HabariLEO, Amir Mhando ambaye hakuwa na mpinzani alipata kura 78 za ndiyo na moja ilimkataa, hivyo kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TASWA. Mwandishi George John wa gazeti la Nipashe alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa chama hicho. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilienda kwa mtangazaji wa Radio One, Maulid Kitenge. Mwandishi wa Kujitegemea, Sultani Sikilo aliibuka Mhazini Mkuu na Mhazini Msaidizi ilienda kwa Mohammed Mkangara. Mwandishi wa Jambo Leo, Onesmo Kapinga aliibuka miongoni mwa wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji pamoja na Zena Chande, Elius Kambili, Grace Hoka, Alfred Lucas na Salum
No comments:
Post a Comment