LONDON,Uingereza
WAZAZI wa mtoto aliyezaliwa mzungu nchini Uingereza wamekubali uamuzi wa wataalamu wa vina saba kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.
Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa wazazi hao Benjamin na Angela wamekubali mtoto huyo wa kike afanyiwe uchunuzizaidi ili kuibaini sababu za kuzaliwa akiwa katika hali kama hiyo.
Mtaalamu wa vina saba kutoka Chuo Kikuu cha London Dkt.Mark Thomas amesema kuwa ana wasiwasi huwenda kuna mchanganyiko wa chembechembe nyeupe na zile na zile zinasobabbisha mtu kuwa na ulemavu wa ngozi albino ingawa uchunguzi wa awali ulionyesha si albino
Baba mzazi wa binti huyo Benjamin kwa upande wake amesema kuwa licha ya kukubali matokeo ya jinsi mtoto huyo alivyo,bado wataendelea kutafuta sababu za mtoto huyo kuzaliwa hivyo.
Mtoto huyo alizaliwa na wazazi weusi ambao ni raia wa Uingereza wenye asili ya Nigeria na inaelezwa kuwa katika familia yao hawana historia ya kuzaliwa mtu wa aina kama hiyo.
Benjamin ambaye ni mshauri wa huduma kwa wateja alisema kuwa alipomuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza alishutuka lakini baadaye akasema kuwa ni mwanaye na anamuamini sana mkewe.
Alisema mkewe ni mwaminifu kwake sana na walihamia nchini humo wakitokea kwa Nigeria miaka mitano iliyopita. BBC
No comments:
Post a Comment