header

nmb

nmb

Saturday, April 3, 2010

SALAAM ZA PASAKA KUTOKA KWA WANA ,prhabari.blogspot.com!!

Mwigizaji akionyesha kazi za Yesu Kristo alizokuwa akifanya alipokuwa hapa Duniani Miaka 2000 Iliyopita
Kwa siku 3 au 3 mfululizo wakristo nchini wanaungana na
wenzao duniani kukumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo
zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Siku hii ni muhimu kwa waumini wa madhehebu hayo kwani
wanaamini ndipo ukombozi wao ulipopatikana kwa damu ya
Yesu Kristo iliyomwagika msalabani eneo la Kalvari.

Kumbukumbu hii ni muhimu kwa waumini hao kwani kifo
na kufufuka Yesu Kristo ni ushindi dhidi ya kifo na mauti.

Wakati tukiungana na waumini hao kukumbuka siku
hii,tunawakumbusha kuzingatia na kushika mafundisho
mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa dini makanisani.

Ni wakati muhimu kwao kujirudi na kuepuka uovu ambao
umekuwa mzigo mkubwa katika jamii na kuiongezea serikali
gharama kwa kuongeza ulinzi huku mahabusu na mahakama
zikijaa wahalifu siku hadi siku.

Viongozi wa dini wana wajibu muhimu wa kusaidia serikali
katika eneo hili kujenga maadili ya jamii ili kuepukana na
uovu.

Kama jamii itaheshimu na kushika mafundisho ya dini,
tunaamini uovu utapungua kama si kwisha kabisa kwani dini
zote zinafundisha tabia njema kwa wanadamu ambalo ni
jambo muhimu kwa maisha ya utulivu.

Tunawakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha wanaweka
ulinzi wa kutosha kwa watoto msimu huu ambao kwa
nyakati fulani yamekuwa yakijitokeza mtukio mengi ya
kusikitisha zikiwemo ajali, wizi,ubakaji,uvutaji bange nk.

Wazazi na walezi pia wanapaswa kuwa macho
wanapowapeleka watoto wao kwenye kumbi za starehe
wakati wa sikukuu ya Pasaka kuhakikisha maeneo hayo ni
salama ili kuepuka matukio yenye madhara kwa watoto .

Kwa nyie wote mnao kwenda kujirusha katika clubs mbalimbali muwe makini na magonjwa ya ngono.

PR Promotion Kupitia safu hii ya prhabari.blogspot.com,Tunawatakia mapumziko mema ya
Pasaka wote Duniani mnao pitia Blog hii!!

No comments:

Post a Comment