header

nmb

nmb

Wednesday, March 17, 2010

LUCA tONI ATOA MPYA YA 2010


Luca Toni ataka kubakia AS Roma
ROME,Italia


MCHEZAJI Luca Toni ana imani kuwa utapatikana muhafaka kati ya timu ya AS Roma na klabu yake ya Bayern Munich ili aweze kuongezewa muda wa kuendelea kukipiga katika klabu hiyo ya mji mkuu wa Italia.


Kwa sasa Toni anaichezea kwa mkopo klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu lakini ana imani kuwa ataendelea kubakia katika klabu hiyo ya Trigoria.


"Mwishoni mwa mwaka nitazungumza na Bayernna AS Roma, lakini sidhani kama kutakuwepo na tatizo katika kufikia makubaliano,"nyota huyo aliliambia gazeti la La Gazzetta Dello Sport.


Pamoja kuelezea mawazo yake ya kutaka kubakia katik

a klabu hiyo mchezaji huyo alizungumzia pia hisia zake katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Italia baada ya timu hiyo ya Giallorossi kupoteza pointi mbili dhidi ya timu ya Livorno.


"Tumepoteza pointi mbili ugenini,ushindi ndiyo ungefungua tena mbio za kuwania ubingwa,"alisema.


Alisema kuwa kutokana na mtokeo hayo itawabidi kushinda mechi zao zote ili kuweka matumaini hao.

No comments:

Post a Comment