Beckhama kukaa benchi miezi sita
TURKU, Finland
TURKU, Finland
UPASUAJI wa msuli wa kisigino cha mguu wa kushoto aliofanyiwa mchezaji David Beckham umeenda vizuri na madaktari waliomfanyia upasuaji kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza wanatarajia kuwa huenda akakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita.
Dkt. Sakari Orava alisema jana kuwa Beckham (34) anatarajiwa kupona vizuri lakini licha ya yote atazikosa fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Juni 11 mwaka huu nchini Afrika Kusini.
“Anaendelea vizuri na aparesheni ilitumia muda chini ya saa moja na ilienda vizuri ,” Dkt. Orava aliliambia Shirika la Habari la Uingereza AP baada ya kumalizika kazi ya upasuaji iliyofanyika katika Zahanati ya Mehilainen iliyopo katika mji wa Turku,Kusini Magharibi mwa Finland.
“Itakuja kumuwia rahisi ndani ya wiki mbili ama tatu zijazo na kisha ataendelea na ratiba za mazoezi taratibu,"aliongeza.
Alisema kuwa mguu hawezi kuwa na mauamivu kwa zaidi ya miezi miwili ama mitatu.
Orava vilevile alisema kuwa itamchukua miezi minne ili aweze kuanza kukimbia na miezi mingine miwili kabla ya kuanza kucheza soka.
No comments:
Post a Comment