header

nmb

nmb

Saturday, July 23, 2016

MABONDIA IDD MKWELA KUPAMBANA NA MWITA MACHAGE KESHO JUMAPILI JULAI 24 TANDIKA





Bondia Idd Mkwela kushoto akiwa na Mwita Machage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya julai 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Idd Mkwela kushoto akiwa na Mwita Machage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya julai 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS



Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na mabondia wake Mohaed Kisua kg 51 iDDi Mkwela kg 61 Vicent Mbilinyi Kg 63 na Shabani Kaoneka Kg 72  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Idd Mkwela atapanda tena ulingoni kesho jumapili katika mpambano wake mwingine wa Kg 61 atakapo mkabili Mwita Machage katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika

akizungumza baada ya upimaji uzito na afya kwa mabondia watakaocheza siku hiyo 

Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema kuwa mabondia wengine waliopima na watagombania ubingw wa taifa ni Imani Mapambano atakaezichapa na Selemani Galile raundi kumi za ubingwa

katika mapambano haya tumeamua kuchukuwa mabondia chipkizi kwa ajili ya kuendelea kuamasisha mchezo wa ngumi sehemu mbalimbali nchini

hususani katika ukanda uhu wa Temeke ambapo tumekuwa tukichezesha vijana wanao chipukia kila wakati

 Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments:

Post a Comment