MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia chombo cha moto Pikipiki Bryan
Capper yuko nchini kwa mwaliko maalum akitoka nchini kwao Afrika kusini
ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha
pia
unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
Akizungumza leo asubuhi katika viwanja vya Coco Beach Jijini Dar es
Salaam ambako ndiko alikoanza kuonesha onyesho lake la kwanza na
kuonesha umahiri wake katika uendeshaji wa pikipiki yupo nchini kwa
kudhaminiwa na Kampuni ya Red Bull, atakuwa nchini kwa ziara ya siku
tatu.
Kesho Jumapili atakuwa katika viwanja vya Mlimani City na Jumatatu atahitimisha ziara yake katika eneo
la Ubungo Tanesco.
Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini Tanzania pia
tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.
Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club , Blagina
Mwihava alisema kwamba wamemleta
mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa
vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.
“Hii itakuwa ni shoo
kwa watanzania ili waweze kuvutika
kucheza mcheo huu wa aina yake .
Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini
maonesho hayo yote ni ya wazi.
No comments:
Post a Comment