header

nmb

nmb

Sunday, November 16, 2014

Maonesho ya wadau wa Gesi na Oil yaendelea mkoani Mtwara



Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Stanbick jana wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya wadau Gesi na Oil yanayoendelea mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wilman Ndile akizungumza na Ofisa wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, Francis Kihinga wakati walipokutana kwenye mkutano wa wadau wa gesi unaoendelea mkoani Mtwara, TSN ni moja kati ya wadhamini wa mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonesho ya bidhaa za wadau mbalimbali wa madini yaliyofanyika sambamba na mkutano huo. Maonesho hayo yalifanyika katika umbi wa Mikutano wa Chuo cha Veta Mtwara wakati Mkutano wa wadau ulifanyika katika hoteli ya Naf.
Afisa Matekelezi wa NSSF mkoani Mtwara, Jamila Mfanga akimkabidhi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile vipeperushi vya bidhaa zake.
Picha na wadau.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiangalia bango la mafunzo ya Chuo Kikuu Huria ambao walifungua chuo chao mkoani humo, nao walikuwa ni baadhi ya waliojitokeza kwenye maonesho hayo pia pembeni yake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Tolly Mbwete.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiwaonesha baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano wa kujadilia masuala ya gesi na Mafuta unaoendelea mkoani Mtwara, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini (TPSF) Godfrey Simbeye pembeni Mwenyekito wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesela.

No comments:

Post a Comment