INATISHA :NYAMA YA BINADAMU YAUZWA HOTELINI, 11 WAKAMATWA
Alhamisi iliyopita polisi walikamata watu 11, baada ya kukuta vichwa 2 vya watu katika hoteli (jina limehifadhiwa ) iliyoko karibu sana na soko maarufu la Ose-Okwodu, katika jimbo la Anambra, Nigeria.
Kwa mujibu wa gazeti la OSUN DEFENDER, katika tukio hilo pia zilikamatwa bunduki 2 aina ya AK47 pamoja na silaha nyingine kadhaa katika hoteli hiyo. Tukio hilo lilifuatia polisi kupewa tip na wakazi wanaoishi karibu na hoteli hiyo.
Mmiliki wa hoteli, wanawake 6 na wanaume 4 walikamatwa. Polisi walipovamia hoteli hiyo walikamata vichwa viwili vikiwa vimefungwa katika mifuko ya plastiki, bunduki 2 aina ya AK47, kofia 2 za jeshi, pamoja na silaha 40 za mauaji na simu kadhaa za mkononi.
No comments:
Post a Comment