HUYU NDIO MKURUGENZI MKUU MPYA WA EWURA
UTEUZI
BWANA FELIX NGAMLAGOSI
Taarifa inatolewa kwa umma kwamba, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha Sheria namba 14(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, Sura Na. 414, Waziri wa Maji, Mhe., Prof., Jumanne Maghembe (MB), ambaye pia ni Waziri anayehusika na EWURA, amemteua Bw. Felix Ngamlagosi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kuanzia tarehe 1 Februari 2014.
Bw. Ngamlagosi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Haruna Masebu, aliyemaliza muda wake tarehe 31 Desemba 2013, baada ya kuitumikia Mamlaka kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja kwa mujibu wa Sheria ya EWURA.
No comments:
Post a Comment