MKE wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mama Aisha Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ‘5th
Extra Vaa Khanga Party’ ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba
8.
Akizungunza jana, mwandaaji wa onyesho hilo, Asia Idarous, alisema
usiku huo Mama Asha Bilal atakuwa mgeni rasmi sambamba na watu mbalimbali
maalufu wa ndani na nje ya Tanzania ambo pia watashuhudia muziki wa bendi ya
Mashauzi Classic na DJ Mkongwe nchini DJ
John Dilinga .
“Wadau wa mitindo watapata burudani na kufurahia mitindo ya
khanga itakayoonyeshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,”
alisema Asia Idarous.
Alisema usiku huo vazi la khanga ndilo litakuwa maalumu kwa
wadau watakaohudhuria sambamba na
kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Onyesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ambalo mwaka huu
limeandaliwa kwa ushirikiano wa Asia Idarous na Fabak Fashions, linatarajiwa
kuwa na shangwe mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na nyota
mbalimbali. Wakiwemo Shilole, Snura, Ben Kinyaiya, Kibonde na wengineo.
Kiingilio katika onyesho hilo ni sh 30,000 na viti maalumu
itakuwa ni sh 50,000 ambako tiketi zimeanza kuuzwa Fabak Fashions Mikocheni na
Gift Shop Serena Hotel.
Aidha, alisema kati ya pesa zitakazo patikana pia zitaenda
kusaidia kituo maalum cha kupambana na waathirika wa dawa za kulevya.
Usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd’s, CXC, Clouds
FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Vijimambo blog,Voice of America,
Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na
Miss Tanzania,New Africa tv.com na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment