Jumamosi, 12 Oktoba 2013
A
KLABU ya Simba leo imeendelea kung’ang’ania kileleni
baada ya kuitandika Tanzania Prisons bapo 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati Simba ikikaa kileleni baada ya kujikusanyia
pointi 18, watani wao Yanga nao wamezidi
kuwakalia kooni baada ya kuinyuka Kagera Sugar wakiwa uwanja wa nyumbani mabao
2-1.
Yanga baada ya ushindi huo wamerudi katika nafasi yao
ya pili baada ya kufikisha pointi 15 hivyo
mchezo wa watani hapo wa jadi wa Oktoba 20 ndiyo utakaoamua nani atakaa
kileleni au kumfikia mwenzake.
Bao pekee la Simba lilifungwa na Jonas Mkude kwa
shuti la mbali nje ya eneo la hatari na kumshinda mlinda mlango wa Prisons Beno
David na mpira kukwama wavuni.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na
Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza wakati bao la Kagera lilikwamishwa wavuni na Godfrey
Wambura.
Mchezo mwingine wa Ligi hiyo uliochezwa kwenye
Uwanja wa Chamanzi Ashanti United walizinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Coastal Union.
No comments:
Post a Comment