header

nmb

nmb

Tuesday, October 15, 2013

PAMBANO LA KARAMA...MAANDALIZI YA NGUMI YAKAMILIKA

 

Maandalizi ya mapambano ya ngumi yanayotegemewa kufanyika  katika ukumbi wa ccm mwinjuma-mwananyamala  ambayo inawezekana yakavunja rekodi ya mapambano mengi kufanyika kwa mara moja kwa mwaka huu kuliko mengine,kwani kuna zaidi ya mapambano 14 makali ya utangulizi.hii itasaidia kwa wale watakaokuwa mpirani wa samba na yanga kuwahi mapambano  makubwa yatakayosalia ambayo ni ya bondia mwenye ngumi za hatari  na mara nyingi huwazimisha wapinzani wake Zumba kukwe au chenji dola kama anavyojiita mwenyewe  wa kibaha atakae zipiga na Ali boznia wa Tanga atakaefuatana na alan kamote na meneja wao ali mwanzoa wakitokea mkoani tanga, mapambano mengine ni  Mwaite Juma na Shadrack ignas hii ni vita kali ya ulingoni wote sugu wote wabishi kushindwa, nae bingwa wa zamani wa bantam  Ajibu salum atapimana ubavu na Martin Richard,huku  mbena Rajab akizipiga na Godwin Mawe, Ibrahim class  na Rashid Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly, mdogo wake francis miyeyusho  Yona miyeyusho  atacheza na julias Thomas, Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa mwananyamala sokoni  joseph stanslaus(amita au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni  shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa mabondia hawa, nae  yasin omari  atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na mapambano  mengine kadhaa ya vijana wadogo wenye vipaji  vya mchezo wa ngumi. Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion  kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche boy) atakaezipiga  na  ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane na SADO PHILEMON ambae anategemewa kuwasili alhamis akitokea songea  atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito wa middle kutafuta mshindi  wa atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani na wanategemea kupima afya zao na uzito siku ya jumamosi saa nne asubuhi hapohapo katika ukumbi wa ccm mwinjuma mwananyamala A.

No comments:

Post a Comment