header

nmb

nmb

Friday, September 20, 2013

SHEREHE YA KUSAINI MABALOZI WA HESHIMA NCHINI MAREKANI.


Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Bernard Membe akitoa hotuba ya kuwapongeza mabalozi wa hiyari wa Tanzania.


Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea machache kuwashukuru Mabalozi wa Heshima kwa kukubali kwao kuitangaza Tanzania nchini Marekani na kusema sio kazi rahisi lakini ana Imani nao na aliwatakia kila la kheri ya kuwa na nia thabiti ya kuitangaza Tanzania nchini Marekani.
 
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatambulisha Waheshimiwa Mabalozi wa  hiyari ndani ya Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Washingto DC
Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Heshima Mhe.  Kjell Bergh kutoka Jimbo la Minnesota  wakiweka saini ya mkataba wa ubalozi wa heshima watakao wajibika kufanya kazi za wakiitangaza Tanzania nchini Marekani,  uwekezaji wa Utalii na kuinua uchumi wa Tanzania
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akimkabidhi mkataba wa Ubalozi wa Heshima Mhe. Kjell Bergh kutoka Minnesota baada ya kuweka saini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataowajibika kufanya kazi za wakiitangaza Tanzania nchini Marekani,  uwekezaji wa Utalii na kuinua uchumi wa Tanzania
Mhe.Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Marekani na Mexico akiweka saini na ballozi wa hiari Mhe. Charles Gray  kutoka Jimbo la Pennsylvania
Waziri wa mambo ya nje Mhe. Bernard Membea kimkabidhi mkataba aliotia saini  Balozi wa hiyari Mhe. Charles Gray  kutoka Jimbo la Pennsylvania, baada ya kuweka saini mikataba ya kuwa rasmi Balozi wa heshima watakao wajibika kuitangaza Tanzania.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa hiyari Mhe. Ahmed Issa kutoka Jimbo la California wakiweka saini ya mkataba wa ubalozi wa heshima .
Waziri wa mambo ya nje Mhe. Bernard Membe akimkabidhi mkataba wa balozi wa hiyari Mhe. Ahmed Issa baada ya kuweka saini mkataba na kuwakilishwa rasmi Mabalozi wa heshima.

No comments:

Post a Comment