Tuzo za vijana walio chini ya umri wa
miaka 30, zimetolewa jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini
Dar es Salaam na kushuhudia vijana nane wakiibuka washindi kwenye nyanja
mbalimbali zikiwemo Mchango kwenye jamii, Ujasiriamani, Uvumbuzi,
Michezo, Burudani, Mitindo na zingine.
Tuzo kubwa ya siku ya Mchango kwenye
Jamii (Social Impact) imechukuliwa na Adam Anthony ambaye ni mkurugenzi
wa DAELIT Group anayejihusisha na masuala ya mazingira.
Akiongea na Bongo5 mara baada ya kupata
tuzo hizo, Adam amesema pamoja na kuwa na furaha kubwa kushinda tuzo
hiyo, bado anahitahi kujitumza zaidi kwakuwa jamii itategemea mambo
makubwa kutoka kwake. “Wakati mwingine unajisikia woga kwamba jamii sasa
inategemea vitu vikubwa kutoka kwako, kwahiyo inazidi kukusukuma ufanye
vitu vikubwa zaidi,” alisema
Tuzo kwa upande wa mitindo imechukuliwa
na Jokate Mwegelo ambaye amesema amejisikia faraja kutambua kuwa kazi
zake zinakubalika na ndio maana wamempigia kura.
Millard Ayo – Media
Richard Kazimoto – Uvumbuzi/Innovation
Ben Pol – Burudani
Ainaso Joakim – Arts and Designing
Michael Mbwambo – Ujasiriamali
Mgeni wa heshima kwenye tuzo hizo
alikuwa ni Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia, Ndugu January Makamba.
Makamba amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kusema kuwa licha ya
kwamba kuna changamoto za hapa na pale, wamefanya kazi nzuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa
Youth For Africa (YOA), waandaaji wa tuzo hizo, Awadh Milasi amesema
kutokana na kutoa tuzo hizo za kwanza, wamejifunza mengi na hivyo
kuahidi kuzikuza zaidi tuzo hizo kwa kushirikisha mikoa mingine na
nyanja nyingine ili kuzipa sura ya kitaifa.

No comments:
Post a Comment