Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri
na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na
Haidom mkoani Manyara, wamelazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo
na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, na kisha
kulichoma moto basi hilo.
Taarifa toka eneo la tukio zinasema
wananchi hao ni wa vijiji vya Singa, Idabagadu na Nkungi mkoani Singida,
ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi
hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.
Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita
No comments:
Post a Comment