Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Isere Sports inayoshuhulika na
uagizaji na uuzaji wa vifaa vya michezo,Abbas Isere (kulia) akimkabidhi
jezi Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko ,Maulid Mtika
maarufu Milulu zenye thamani ya Sh. 350,000.
Isere sports yatoa jezi kwa timu ya Kilwa Masoko
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Vifaa vya michezo, Isere Sports imetoa jezi seti moja yenye thamani
ya sh. 350,000 kwa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko inayoshiriki Ligi
Daraja la Tatu wilaya ya Kilwa.
Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga, Maulid Mtika akipokea jezi hizo
jana alisema msaada huo ni mfano wa kuigwa na wafanyabiashara wengine
wenye uwezo wa kusaidia kuibua vipaji vya vijana kwenye soka.
Mtika
ambaye ni maarufu kwa jina la Milulu alisema imefika wakati Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) litafute njia ili lishuke mpaka ngazi ya wilaya
kujua matatizo yanawakabili timu ili kutafuta vipaji vya wachezaji
watakaochukua nafasi ya waliopo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
'Tunao vijana wenye vipaji vya kucheza soka kufikia ngazi ya timu ya
taifa, kinachowanyima nafasi ya kuonekana ni vifaa vya michezo tunaomba
TFF ishuke mpaka ngazi ya wilaya kuwasaidia vijana kukuza vipaji.
Alitoa
wito kwa wadau wa michezo kujitokeza kusaidia timu ambazo hazina
wafadhili lakini kuna vijana ambao wako tayari kuonesha vipaji vyao
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema jana kuwa
msaada huo ameutoa ili kukuza vipaji vya soka katika wilaya hiyo ambao
wanahitaji misaada kama hiyo ili kuendeleza vipaji.
No comments:
Post a Comment