header

nmb

nmb

Monday, June 17, 2013

Timu ya Mpira wa Miguu ya Konyagi yaibuka kidedea


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge

Timu ya Mpira wa Miguu ya Konyagi jana iliibuka kidedea baada ya kuifunga  Timu ya Bunge Sports Club bao tatu kwa bila.
Mchezo huo umechezwa jana katika kiwanja cha Jamhuri mjini Dodoma.
Bao la kwanza la  timu ya Konyagi lilifungwa ndani ya dakika 14  baada ya mchezo kuanza ambapo Hassan Luiza alitia nyavuni goli hilo baada ya kuwapiga chenga kali wachezaji wa timu ya Bunge.
Mchezo huo haukuwa mzuri kwa timu ya bunge  baada ya mchezaji Hassan Nyange kuipatia timu yake  bao la pili katika dakika ya 15 huku Aman Salum akiingizia  timu yake bao la tatu katika dakika ya 18.
Wakati huo huo Bunge Sports Club imeibuka mshindi baada ya kuifunga bao moja timu ya Benki ya NMB.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 25 katika kipindi cha kwanza baada ya mchezaji wake Yusuph Gogo kuruka vihunzi vya wachezaji wa NMB.

No comments:

Post a Comment