header

nmb

nmb

Monday, June 17, 2013

TDL imetoa msaada wa vyerehani 25 vyenye thamani ya shilingi milioni 5

 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya BNaibu Spika wa Bunge, Job Ndugai


KAMPUNI  Konyagi Tanzania (TDL) imetoa msaada wa vyerehani 25 vyenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa wanawake wasio jiweza wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Msaada  huo umekabidhiwa jana mjini Dodoma na meneja mauzo JOSEPH CHIBENE kwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo WHITE ZUBERI. 

CHIBENE amesema lengo la msaada huo ni kuwasaidia wakina mama hao ambao kipato chao ni cha chini sana ili waweze kuinua kipato chao na kujikwamua kiuchumi.

Amesema TDL  inatoa huduma kwa jamii na ili washirikiane vizuri na Jamii hiyo ni vizuri kugawana katika mapato wanayopata kupitia misaada mbalimbali wanayotoa.

Kwa upande wake mwenyekiti ZUBERI ameishukuru TDL kwa msaada huo utakaotumika kuwaendeleza wakina mama kiuchumi.

Amesema msaada huo unadhihirisha namna TDL ilivyokuwa karibu na jamii na kuomba makampuni mengine yanayofanya biashara nchini kuiga mfano huo.

No comments:

Post a Comment