header

nmb

nmb

Tuesday, May 28, 2013

MJI MPYA WA KIGAMBONI



Waziri wa ardhi Mhe.Bi Anna Tibaijuka ameliezea bunge kuwa nyumba takribani elfu 30 zitajengwa na makampuni ya Dubai na Wachina, na wakazi wa Kigamboni watakuwa na hisa ! Kauli hiyo ya waziri Anna Tibaijuka inawatia wasi wasi wananchi na kujiuliza maswali mengi kama vile kuwa na hisa katika biashara hipi? nani mmiliki wa Ardhi? mbona wananchi wa Kigamboni hawajapewa taarifa yoyote!  hakuna kikako chochote kile kilicho washirikisha wananchi na kujua hatima yao ! mbuge wa Kigamboni Mhe.Ndugulile naye kashangazwa na kauli ya Waziri.
 Wenyeji wa asili ya mikoa ya Dar-es-salaam na Pwani, wamejawa na unyonge na kujiona wapo katika kilio cha kusaga meno kwa kuondolewa katika sehemu zao za asili na kutojua wapi watapelekwa,Tabia za baadhi ya wajanja kumiliki mashamba makubwa nalo limekuwa ugonjwa ulijitokeza katika kumiliki Ardhi.
   
   UVUNJWAJI WA SHERIA ZA ARDHI
 Migogoro mingi ya Ardhi inatokana na uvunjwaji wa sheria zilizopo na wizara inahusika kwa namna moja au ingine katika kuvunja sheria hizo, Kuna Ardhi zinazomilikiwa kimila,pia na manispaa, lakini Wizara ya ardhi imekuwa ikiwanyang'anya wazawa na kuwapa wawekezaji wa kigeni ardhi hizo bila ya kuwashirikisha wahusika,wananchi,serikali za mitaa na manispaa. Ni juzi tu wakazi wa eneo la Tuangoma, njia panda ya Amani beach huko  Kimbiji walijikuta wanabobolewa majumba na kulazimishwa kulipwa fidia la Sh.700,000 kwa heka ! na muwekezaji wa Kichina ndio kaanza kazi? Wanajeshi nao wanajaribu kuwatishia maisha wanye mashamba  ili wapate mashamba ya bure. Serikali ilitupia jicho tatizo la Ardhi tusije tukawa watumwa katika nchi yetu.

No comments:

Post a Comment