header

nmb

nmb

Wednesday, March 6, 2013

DR Mwinyi amtembelea Kibanda Muhimbili Baada ya Kupigwa na watu wasio julikana!!





Waziri wa Afya, Dk Hussein Mwinyi leo asubuhi amemtembelea kumjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda aliyelazwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari ambao pia wanachapisha magazeti ya michezo ya Dimba na Bingwa, usiku wa kuamkia leo alishambuliwa na watu wasiojulikana.


Ingawa watu hao wanaaminika kuwa ni majambazi, lakini imeelezwa hawakupora kitu chochote ndani ya gari lake, mfano simu na kompyuta mpakato (laptop).




Kibanda aliumizwa na watu hao ambao walimvamia wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam. Wakavunja kioo cha gari na kumtoa nje kabla ya kuanza kusmhambulia ikiwa ni pamoja na kumkata mapanga kichwani na kulijeruhi vibaya jicho lake, pia imeelezwa wamemyofoa kucha.


Kibanda ameumizwa vibaya jichoni, tayari madaktari wameonyesha hofu ya jicho hilo kurudi katika hali yake ya kawaida na uwezo wa kuona tena. Hata hivyo wamekuwa wakiendelea na juhudi.

Kabla ya kurejea New Habari, Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Free Media wanaochapisha gazeti la Tanzania Daima na Sayari, kabla ya hapo alikuwa Mwananchi Communications.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Ndugu Absalom Kibanda akiwa hospitali ya taifa ya muhimbili muda mfupi baada ya kuvamiwa na kupigwa vibaya na watu wasiojulikana.picha hii imepigwa saa tisa usiku wa leo na Mdau Chongoloh
---  ABSALOM KIBANDA AVAMIWA NYUMBANI KWAKE NA KUTOBOLEWA JICHO
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kibanda alivamia majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.

Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.

Watu waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.

Blog ya Kamanda wa Matukio imesikitishwa sana na unyama huo aliofanyiwa mpiganaji Kibanda na inaomba vyombo vya Dola vifanye jitihada za ziada kuwabaini wale waote walihusika na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

Pole saaaana mpiganaji wetu Kibanda, Mungu atakujalia upate matibabu na kupona haraka.
 

No comments:

Post a Comment