header

nmb

nmb

Tuesday, March 26, 2013

ANASWA KWA KUJIFANYA BUBU IRINGA NA KUOMBA PESA

 

Huu ndio  ujumbe ambao tapeli huyo anatumia  kuombea  pesa unasomeka  kuwa  mimi ni bubu nisaidie nauli  ya  kurudi kwetu Mbeya
Hapa baada ya  kufika  eneo la Dragon bar usiku  wa  leo kutaka  kutapeli na kubainika kuwa si bubu baada ya  kupewa  kibano na kuongea kwa anaomba kusamehewa
kijana Maron Benjamin Mbilinyi mwenyeji  wa Chimala  wilaya ya Mbarali mkoa  wa Mbeya anayejifanya ni bubu kumbe tapeli 
Bw  Jumanne Juma (kushoto)  Said kulia  wakimtazama kijana  huyo baada ya  kupewa  kibano na kuwaimbia wimbo kijana  huyu  kati ni Maron Benjamin Mbilinyi.alijifanya ni bubu
 
 
Hapa  wakimtoa katika chumba walichombana na kuzungumza  kuwa yeye si bubu 
Hapa akitoka katika  chumba  hicho  baada ya  kibano usiku huu
Shida ni kipimo cha akili usemi huu  ni  kweli kabisa kijana Maron Benjamin Mbilinyi.mwenyeji  wa Chimala wilaya ya Mbarali mkoa  wa Mbeya  amenusurika  kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya  kukutwa akizunguka mitaani  kuwatapeli fedha  wakazi  wa  mji wa Iringa kwa kisingizio  kuwa ni bubu asiyeweza  kuongea .

Mtandao huu  wa ww.francisgodwin.blogspot.com  umeshuhudia kijana huyo Maron Benjamin Mbilinyi akipewa  kibano baada ya  kufiika eneo la baa maarufu ya DRAGON iliyopo eneo la TFA na  kuwaomba  wateja wa eneo hilo kwa  kutumia ujumbe  mfupi aliouandika katika karatasi aina ya tishu akieleza  kuwa yeye ni bubu anaomba  kusaidiwa nauli ya  kurejea kwao Mbeya .

Baada ya uchunguzi  wa haraka uliofanywa na wanachi hao  kwa kushirikiana na mwandishi  wa mtandao  huu kwa  kumvuta kijana huyo pembeni na kumweka kati ndani ya  chumba kimoja katika baa hiyo ndipo alipoanza  kukunjua makucha yake na kuomba asipewe  kipigo na badala yake kuwaomba  watulie  ili  awaimbie  wimbo mmoja mzuri  aliouimba kwa lugha ya  kimbombo na kuwafanya kumuhuji sababua ya kujifanya  bubu.

Kijana  huyo alisema kuwa amepata  kutumia njia  hiyo katika mkoa  wa Ruvuma ambako  pia alishitukiwa na  wanahabari kama  ilivyojitokeza  leo mjini Iringa na mkoani Mbeya pia .

Hata  hivyo amesema amepata kuwapiga mziga watu mbali mbali  wakiwemo viongozi  wa serikali ambao  pia  wamepata  kuamini kuwa ni bubu na kumpata msaada  wa  pesa na kuwa kila siku amekuwa akikusanya zaidi ya Tsh 50,000 hadi 100,000 kutoka kwa  wananchi mjini Iringa .

Kijana  Maron Benjamin Mbilinyi amesema kutoka na kuwa mbinu  hiyo imegundulika mjini Iringa anategemea kuhama katika mji  wa Iringa na kwenda katika mkoa mwingine  kuendelea na libeneke la  kuomba kwa kujifanya  bubu na kuwataka wanaotaka  kuiga mbinu  hiyo  kuwa na moyo mgumu kwani kipigo ni nje nje pale  inapobainika  kuwa si bubu  kweli .

No comments:

Post a Comment