
Diwani
Kata ya Kwadelo Kondoa mkoani Dodoma Alhaji Omar Kariati akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa hafla ya wakulima wa kata hiyo
kukabidhiwa matrekta mannem kwenye Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es
Salaam, leo. Julai 26, 2012.

Diwani
wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo za
trekta, mkulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani, katika hafla ya
diwani huyo kukabidhi matrekta manne wakulima kutoka kata hiyo, kwenye
Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT,
Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao
kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana
kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja
ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa
kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha
miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni wakulima wa kata
hiyo ya Kwadelo, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (wapili kushoto) na
Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.

Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan akisalimiana na
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omar Kariati wakati wa
hafla ya wakulima wa kata hiyo kukabidhiwa matrekta mannem kwenye
Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es Salaam, leo. Julai 26, 2012.

Mkulima
wa Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Gaberiel Galahenga akimkabidhi barua
Diwani wa Kata hiyo, Omari Kariatikwa ajili ya diwani huyo kumpelekea
kama shukurani Mkuu wa JKT, kwa shirika la Suma JKT kuwawezesha
wakulima wa kata hiyo kukubali kuwapa mattekta wakulima wa kata hiyo
kwa nusu ya bei na kisha kumalizia pole pole. Wengine katika picha
ni, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (watatu kushoto) na Meneja wa
Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.

Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto)
akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani
(kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta
manne, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012.
Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina
trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani
Kariati. Trekta moja ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao
wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki
katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.
No comments:
Post a Comment