Monday, June 18, 2012
ITANIWIA VIGUMU KUKUSAHAU WILLY EDWARD OGUNDE
Marehemu Willy Edward (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
MIMI KAMA SPEAR PATRICK Ilikuwa nni vigumu kuamini Msg ya Bw. Peter Mwenda iliyoingia wakati niko kitandani ikisema Willy Edward Mhariri wa Jambo Leo Amefariki dunia morogoro usiku wa kuamkia leo
Nilinyanyuka kwa machungu makubwa na kumpigia sim mwenda bila ya mafanikio na kumtafuta Amiri Mhando ambaye alinifariji kuwa kila nafsi itaonja mauti
Pia nita mkumbuka Willy Ogunde kwa mengi maliyo nifanyia nami pia niliyo mfanyia tangu tukiwa tunafanya kazi katika Gazeti moja la Majira na hadi alipo ondoka kwenda Jambo leo Bado alikuwa ni Msaada kwangu
Muda wa Mwisho Kuonana na Mdogo angu Willy Ilikuwa ni Miss Tabata ambapoi aliongozana na Mkewe na Mimi nikamuonaz kwa mbali ndipo nilipo mpigia simu na kuanza kumtania kuwa nimemuona ameongozana na Mzigo na yeye akanijibu kuwa haukuwa mzigo ni Mkewe
Muda wa Mwisho Kuonana na Mdogo angu Willy Ilikuwa ni Miss Tabata ambapoi aliongozana na Mkewe na Mimi nikamuonaz kwa mbali ndipo nilipo mpigia simu na kuanza kumtania kuwa nimemuona ameongozana na Mzigo na yeye akanijibu kuwa haukuwa mzigo ni Mkewe
"Yaani we Spear Unamwita mke wangu mzigo we mwenyewe kasikia"tukacheka na kumwambia huu ni usiku na huko ni mbali sasa nipe nimwombe radhi na kufanya hivyo nami nika mwomba radhi mkewe kisha kucheka saaaaana muda mfupi kabla ya kabla ya mwandaaji wa Miss Tabata Fred Ogot kuja kutuchukua ilituingie ndani ya Ukumbi wa Dar Westi aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Willy Mungu ametenda apendavyo baba tangulia.
Nasema sikujua kwa kuwa niliyasema kwa utani wakati tulipokuwa tukiagana ingia kuangalia Michuano hiyo ya urembo.?
Karedia baada ya kupokea simu yangu, aliniambia kwa sauti ya kunyong’onyea akisema, “Kamanda, Willy Edward hatunaye tena, nimejaribu kukupigia lakini simu yako nimekuwa siipati”.
Nilijikaza kumsikiliza Karedia huku nikibubujikwa na machozi, akanieleza kuwa Willy alikwenda kuwaona watoto wake na alikuwa huko hadi saa sita usiku, na kisha alimwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo la kurejea katika hoteli alikokuwa amefikia.
Lakini baada ya kutoka nje, kabla ya kupanda pikipiki alidai anasikia kizunguzungu na kisha alianguka.Wenzake walijitahidi kumkimbiza hosipitali lakini walipofika na kufanyiwa vipimo daktari aligundua tayari alikuwa ameshafariki dunia.
Hivyo ndivyo alivyozimika ghafla Willy Edward, ambaye mashabiki wa michezo watamkumbuka daima kama mpenzi wa mpira wa miguu na zaidi shabiki wa kutupwa wa Klabu ya Yanga kwa hapa nchini na Arsenal kwa timu za nje.
Pia Willy alipenda sana muziki wa dansi, ule wa zamani na huu wa kisasa, akiwa mshirika wa karibu wa bendi ya Twanga Pepeta, ambayo amefanya nayo kazi pia kwa muda kadhaa.
Kwa muda wote wa miaka miwili na miezi mitatu niliyokaa naye Jambo Leo, nilimfahamu kwa undani na kutambua kuwa alikuwa mpole, mtaratibu na mkimya, aliyependa kusikiliza na kujifunza zaidi kabla ya kutenda au kuzungumza.
Willy alikuwa mchangamfu, mwepesi wa kuelekeza na mwenye kupenda ushirikiano na watu wengine. Alikaripia na kuonesha hasira pale ambapo ililazika kufanya hivyo lakini haikuwa hulka yake.
Pamoja na kubadilishwa nafasi kutoka mhariri wa michezo kuwa habari na kisha Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Willy alibakia kuwa yule yule mwenye silika ya upole na ushirikishaji wa wenzake asiyependa kujivuna.
Willy alipenda kukuza lugha ya Kiswahili kupitia tasnia ya habari, na katika kufanya hivyo kila mara alipenda kufanya kazi akiwa na kamusi ya Kiswahili pembeni, akichukua baadhi ya maneno na kuyatumia kwenye gazeti mara kwa mara kama misamiati mipya ambayo baadaye ilizoeleka.
Yako mengi ya kuandika kumhusu Willy Edward, ambaye sasa ni marehemu lakini itoshe kusema kuwa tumepoteza mtu muhimu katika tasnia ya habari na fani nyingine kama michezo na muziki.
Mungu ametoa na ametwaa, jina lake lihimidiwe. Tunamwomba ailaze pema peponi roho ya mwenzetu Willy Edward Ogunde. Lakini kwangu itanichukua muda kumsahau kaka yangu huyo.

No comments:
Post a Comment