Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki akizungumza na vyombo vya habari wakati wa zoezi la kubandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuendesha +simu =kifo, zoezi hilo
limefanyika jijini Dar es Salaam.
Kamanda Jeshi laPolisi Kikosi cha Usalama barabarani SACP Mohamed Mpinga, akibandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na club ya Rotary yenye ujumbe wa kuendesha +simu =kifo kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi, kulia ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia zoezi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki akishirikiana na viongozi wa usalama barabarani akibandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary ya
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki (wa tatu kutoka kulia mwenye miwani) akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamoja na viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia siku za mkononi. Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani SACP Mohamed Mpinga, muwakilishi kutoka Club ya Rotary Dar es Salaam, Bw. Zainul Dossa pamoja na Bw.
Hamza kassongo.
SERIKALI imesemakutokuwepo kwa sheria ya barabarani inayozuia matumizi ya simu za mkononi
wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto kunachangia kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva ambao waonekana kutumia simu za mkononi huku wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Hamis kagasheki wakati wa zoezi la kubandika ujumbe katika magari mbalimbali unaokataza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto.
"Ni kweli hadi sasa hakuna sheria inayomkataza moja kwa moja dereva kuacha kutumia simu awapo barabarani lakini naomba wananchi wafahamu kuwa hili linafanyiwa kazi na wafuate maelekezo yalioyotolewa na wadau kama hawa ambayo kiukweli yanatoa elimu ya kupunguza madhara ya ajali za mara kwa mara" alisema Balozi Khagasheki.
kwa mujibu wa tathmini ya jeshi la polisi baadhi ya ajali nyingi zinazotokea barabarani zinatokana na matumizi ya smu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto hali inayopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi na kusababisha vifo ambavo vingeweza kuzuilika kwa urahisi.
Balozi kagasheki amesema kuwa upungufu wa kutokuwa na sheria ya kuzuia matumizi ya simu za mkononi wakati kuendesha gari unapelekea kushindwa kuwachukulia hatua kali madereva ambao wanaonekana kufanya hivyo.
Naye muandaaji wa zoezi
matinde afisa uhusiano wa kampuni ya smu za mkononi ya Airtel wamesema kuwa zoezi
Zaidi ya machapisho elfu 5 yametengenezwa kwa ajali ya kubandika pamoja na kusambazwa katika magari mbalimbali ambayo yatarahisisha kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuilika kwa kshirikiana na jeshi la polisi.kwa hisani ya kamanda Mpinga wa Jeshi la Polisi nchini
No comments:
Post a Comment