Safari ya mwisho ya Whitney
Usiku wa mwisho wakati Whitney akiponda raha
Whitney akiondoka klabu ya usiku ya Tru, siku moja kabla ya kifo chake
Gari aina ya Golden Hearse lililobeba mwili wa Whitney Houston likiwasili New Jersey
Vyombo vya vyakula vikiwa bafuni
Bafu la kifahari katika hoteli aliyofia Whitney
Chakula cha mwisho alichokula Whitney kabla ya mauti
Mumewe Bobby Brown marufuku kufika msibani
* Alisema kwamab 'hakika anataka kumuona Yesu'
* Mwili wake wawasili nyumbani, atazikwa Ijumaa
* Polisi walimkuta na chupa sita za vidonge bafuni
* Kabla ya kifo alibugia chipsi, hamburger, sandwich
NEW JERSEY, Marekani
MWILI wa mwanamuziki nguli duniani aliyefariki Jumamosi katika Hoteli ya Beverly Hilton, Whitney Houston, umewasili nyumbani kwake tayari kwa taratibu za shughuli za mazishi.
Watu wa karibu na Whitney wamebainisha kwamba mwanadada huyo alijitabiria kifo kwa kusema kwamba 'hakika alitaka kumuona Yesu' siku moja kabla ya kifo chake.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.com ya Marekani, Whitney alikuwa akinukuu vifungu vya Biblia vilivyowahusisha Yohanna Mbatizaji na Yesu, huku akiimba siku moja kabla ya kifo chake.
Imeripotiwa kuwa Ijumaa, aliimba wimbo wa Jesus Loves Me wakati akitumbuiza kwenye klabu ya usiku ya Tru iliyopo Hollywood, na alimwambia mmoja wa marafiki zake: "Nakwenda kumuona Yesu - nataka kumuona Yesu."
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwili huo uliwasili nyumbani kwake Whigham kwa ndege binafsi na taratibu za mazishi zilikuwa zikiendelea na kubainisha kuwa mazishi yatafanyika Ijumaa.
Taarifa zinadai kuwa huenda malkia huyo wa Pop na R&B alifariki kutokana na ugonjwa moyo ambapo inaaminika kuwa kiasi kidogo cha maji kilikutwa katika mapafu yake.
Polisi wa Los Angeles wamesema walikuta chupa sita za vidonge vinavyofahamika kama Xanax, Lorazepam, Ibuprofen, Midol, Amoxicillin na Valium.
Picha zimeonesha matukio kadhaa vikiwamo vyakula alivyotumia usiku akiwa na washikaji zake kabla ya mauti kumfika nguli huyo na miongoni mwa misosi hiyo ni pamoja na chipsi, hamburger, sandwich na jalapons.
Inasemekana kuwa alipokula aliingia bafuni na kuchukua muda mrefu na moja ya picha inaonesha vyakula hivyo vikiwa bafuni huku glasi tupu ya shampeni pamoja chupa ya bia vikiwa katika meza aliyokuwa amekaa awali.
Tetesi zinasema kuwa mwanamama huyo alikuwa na desturi ya kutembea na vipodozi ili kuweka ngozi yake katika hali ya kuvutia, pia taulo na vibanio vya nywele vilikutwa bafuni humo.
Polisi wanasema wanapeleleza ili kujua mtu aliyehusika katika kumpa dawa kabla ya kifo chake na hii ni kama ilivyokuwa katika kifo cha Mfalme wa Pop, hayati Michael Jackson, ambaye daktari wake, Conrad Murray alihukumiwa kifungo.
Dunia yamlilia tuzo za Grammy
Katika tuzo za Grammy ambazo zilitangazwa na rapa nguli wa Marekani LL XCool J, washiriki wawili wa tuzo za Grammy wamemkumbuka hayati Whitney.
LL Cool J alifungua tuzo hizo kwa sala ya kumuombea, alisikika akisema 'Mwanamke tuliyempenda, dada yetu aliyeanguka' na wageni waliinamisha vichwa vyao na wakati huo alisema sala zao zipo kwa mama yake, binti na wengine waliompenda.
Rapa huyo alisema ingawa ameondoka mapema, bado wamebaki wakiwa wamebarikiwa kwa roho yake yenye uzuri wa kupendeza.
Heshima na sala hizo zilifuatiwa na picha za video yake wakati wa tuzo kama hizi mwaka 1994 ambapo alitumbuiza kwa wimbo wake uliomtambulisha vilivyo wa 'I Will Always Love You' na baadaye kuimbwa na mwimbaji Jennifer Hudson.
Naye nguli wa muziki wa Country ambaye wimbo huo uliandikwa na kuimbwa naye mara ya kwanza, alisema kama wengine naye ameshtushwa na kifo hicho lakini anaamini kuwa bado Houston ataendelea kuishi katika muziki wake aliouacha.
Pia nguli mwingine, Pau McCartney aliyetesa na kundi la The Beattles ambaye aliwahi kushiriki vilivyo na Wacko Jacko katika ngoma ya The Girl is Mine, aliwasha mshumaa na kuweka mashada ya maua.
Tamasha la Grammy lilizoa watazamaji wa televisheni wapatao milioni 39 ambapo ni jambo la kihistoria kwa mwaka huu kwa kuwa walikuja maalumu kwa ajili ya kumkumbuka Houston.
Mwanamuziki Celine Dion (43) alisema kuwa anaamini mihadarati imechukua maisha yake na kubainisha kuwa anahofia dawa za kulevya na kuogopa kutoka 'out' kuhofia kutumia dawa hizo.
Whitney Hoston amefriki akiwa ameweka rekodi ya kushirikiana na wanamuziki kochokocho katika nyimbo mbalimbali kama vile Mariah Crey, Wyclef Jean, Ted Pendergres, Kelly Price, aliyekuwa mume wake Bobby Brown, Deboraha Cox, Miss Elliot na Akon.
Wakati huo huo, mume wa zamani wa Whitney, Bobby Brown ameambiwa kuwa hapaswi kuhudhuria mazishi ya mwanamke huyo.
Mwimbaji wa R&B, Bobby inaelezwa kuwa amefadhaishwa baada ya kusikia habari kutoka kwa watu wa karibu yake wakiwanukuu watu wa familia ya Whitney wakimtaka asihudhurie mazishi.
Bobby ni baba wa mtoto wa kike aliyezaa na Whitney mwenye umri wa miaka 18, Bobbi Kristina, anayelelewa na mama wa kambo, Clive Davis.
Ciao...
Bobby Brown
Chini; Whitney akiondoka klabu ya usiku ya Tru, siku moja kabla ya kifo chake
No comments:
Post a Comment