header

nmb

nmb

Wednesday, February 8, 2012

WAKAZI WA KIJIJI CHA KAPUNGA - MBARALI MKOANI MBEYA WAMEINGIA HASARA YA SHILINGI MILIONI 718.










Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo.

*****

Habari na Mwandishi wetu.


Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameingia hasara ya shilingi milioni 718 kutokana na mwekezaji wa mashamba ya Kapunga rice project kumwaga sumu ya kuua mimea, kwa kutumia ndege.






Mwekezaji huyo alifanya tukio hilo Januari 12 hadi 14, mwekezaji kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa alimwaga sumu hiyo katika mashamba yake, pia na katika mashamba ya wananchi katika eneo linalofahamika kwa jina la Mpunga mmoja, na kusababisha wakulima zaidi ya 154, wanaomiliki zaidi ya hekari 494 na heka 5.





Meneja Mkuu wa shirika la Kapunga Rice Project Wally Vermaak amesema ataendelea kufanya hivyo hadi hapo wananchi hao watakapo acha kutumia ardhi anayoimiriki.





Hadi sasa ni wananchi Baadhi ya wananchi 8 akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Raphael Moreli mwenye umri wa miaka 44 wameshaathirika na sumu hiyo.





Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbarali Luteni Kosimasi Kayombo amesema tume aliyoiunda kuchunguza tukio hilo bado inaendelea na uchunguzi. Chanzo; Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment